Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea hupoteza dola bilioni 21 kwa kutohimiza elimu kwa wasichana:UNFPA

Nchi zinazoendelea hupoteza dola bilioni 21 kwa kutohimiza elimu kwa wasichana:UNFPA

Nchi zinazoendelea kote duniani zingepata mgao wa dola za kimarekani bilioni 21 ikwa wasichana wenye umri wa miaka 10 wangeweza kumaliza elimu ya sekondari.

Hii ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA katika ripoti yake kuhusu hali ya idadi ya watu duniani kwa mwaka 2016.

Ripoti inaonyesha kwamba idadi ya wasichana wanaomaliza shule ni ndogo ikilinganishwa na ile ya wavulana na kwamba wanakabiliwa na ndoa za utotoni, ajira na ukeketaji.

Richard Kollodge ni mahariri wa ripoti hii ya kila mwaka na katika mahojiano redio ya Umoja wa Mataifa anaeleza kwanini ni muhimu watoto wa kike kuwa shuleni.

(SAUTI RICHARD)

‘Sababu ya msingi ni kwamba ni haki yao kuhitimu, faida nyingine ni pamoja na kipato cha juu, ripoti inasema kwamba kwa kila mwaka wa nyongeza msichana anapokuwa shule ya sekondari, muda wake wa kipato unaongezeka kwa asilimia 11 au zadi.’’