Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

NORWAY yawezesha UNRWA kusaidia wakimbizi wa Syria

NORWAY yawezesha UNRWA kusaidia wakimbizi wa Syria

Nchi ya Norway imeongeza mchango wa dola millioni tano na nusu kwa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada wakimbizi wa Palestina UNRWA, ili kusaidia wakimbizi wa Syria. Sasa mchango wa Norway kwa mwaka wa 2016 umefikia dola milioni 10.3.

Hii ni baada ya ziara ya siku mbili ya Pierre Krähenbühl kamishna mkuu wa shirika hilo nchini Norway ambapo alikutana na waziri wa mambo ya nje Børge Brende; Mjumbe maalum kwa mchakato wa amani Mashariki ya Kati, Tor Wennesland,na Katibu Mkuu wa Baraza la wakimbizi nchini Norway Jan Egeland, watafiti kuhusiana na taasisi Fafo; wajumbe wa kamati ya kudumu ya mambo ya nje na ulinzi Storting na mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali.

Miongoni mwa mambo waliyojadili ni ushirikiano wao na hali ya sasa inayokabili wakimbizi wa kipalestina ikiwa ni pamoja wale walioathirika na vita vinavyoendelea huko Syria na vizuizi katika ukanda wa kwa Gaza. Bwana Krähenbühl ameishukuru serikali kwa mchango wao akisema Norway imekuwa mshirika wa thamani kwa UNRWA, na ziara hii inampa nafasi ya kuimarisha ushirikiano huo.

Katika mwaka 2015, nchi ya Norway imekuwa miongoni mwa wafadhili 10 wa juu kwa mipango ya msingi ya shirika hilo. Mbali na michango yao kwa mfuko wa dharura, Norway pia imechangia dola milioni 13.8) kwa mipango ya UNRWA.