Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haiti hali mbaya, kipindupindu kimeshamiri: Nabarro

Haiti hali mbaya, kipindupindu kimeshamiri: Nabarro

Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa licha ya juhudi za uokozi, kufuatia kimbunga Matthew kilichoipiga Haiti karibu majuma mawili yaliyopita, takribani watu laki tano bado wako katika sintofahamu kutokana na kukosa chakula, maji, haduma za afya, malazi na mahitaji mengine muhimu. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

David Nabarro ambaye anaongoza harakati za Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu nchini Haiti, na yuko nchini humo kwa siku ya nne sasa ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa uratibu wa namna ya kuwafikia wahitaji unakwamisha na suala kwamba mawasiliano ni magumu hususani vijijini na kwamba asilimia 15 ya eneo lililoharibiwa bado linahitaji msaada.

Kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu, Nabarro amesema.

( SAUTI NABRRO)

‘‘Tumeshuhudia visa vya kipundupindu kila tunapokwenda, tusichokifahamu ni kwamba kuna visa vingapi, hatujaweza kufika vituoni, ndio maana tunahitaji taarifa zaidi toka pembezoni mwa nchi.’’