Skip to main content

Ajenda ya miji inajali ustawi wa wahamiaji: IOM

Ajenda ya miji inajali ustawi wa wahamiaji: IOM

Ajenda mpya ya miji iliyopitishwa kwenye mkutano wa makazi yaani HABITAT 111 itatoa fursa ya kuimarisha usimamizi wa wahamiaji kwenye serikali za mitaa kwa utaratibu na ujuzi, limesema shirika la kimataifa la wahamiaji IOM.

IOM katika taarifa yake kuhusu fursa za wahamiaji kwenye ajenda hiyo, imesema ni mujarabu kwa kundi hilo licha ya kujali hali, na makazi yao.

Kupitia ajenda hii, nchi wanachama zitaweka ahadi ya kuheshimu kwa ukamilifu haki za binadamu na namna ya kuwahudumia wakimbizi, wakimbizi wa ndani na wahamiaji bila kujali hadhi zao, imesisitiza IOM.

Shirika hilo la wahamiaji limeongeza kuwa nchi wanachama zitaweka ahadi ya kuimarisha umoja kati ya uhamiaji kimataifa na maendeleo kwa kuhakikisha usalama, sheria na ustawi wa sera za uhamiaji.