Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OECD yaahidi dola bilioni 100 kila mwaka kusaidia masuala ya tabianchi

OECD yaahidi dola bilioni 100 kila mwaka kusaidia masuala ya tabianchi

Ripoti mpya kutoka kutoka shirika la ushirikiano wa kuchumi na maendeleo, OECD imenukuu nchi zilizoendelea zikisema kuwa zitachangia dola bilioni 100 kila mwaka kwa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwenye nchi maskini. Flora Nducha na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Flora)

Tovuti ya miradi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi imesema ahadi hiyo ni moja ya makubaliano yaliyomo kwenye mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi uliotiwa saini mwaka jana.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Australia na Uingereza imesema OECD ina uhakika kuwa wanachama wake watafanikisha ahadi ya fedha hizo na watazitoa kutoka vyanzo mbali mbali na hivyo kuahidi kuwa itatekelezwa.

Takwimu zinaonyesha ongezeko la kiwango cha uchangiaji ambapo mwaka 2014 nchi tajiri zilichangia dola bilioni 62 ikilinganishwa na dola bilioni 52 kipindi kilichotangulia.