Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kuboresha lishe Pakistan

WFP kuboresha lishe Pakistan

Shirika la Mpango wa Chakula duniani, WFP kwa kushirikiana na serikali ya Pakistan limezindua mpango wa kuboresha lishe mjini Karachi unaoitwa SUN.

Kwa mujibu wa taarifa ya WFP kuhusu mpango huo katika jimbo la Sindh, SUN unawaleta pamoja juhudi za asasi za kiraia ,wafadhili wafanyabishara , watafiti ambapo kukabilina na utapiamlo hususani kwa akina mama na watoto.

WFP inasema harakati hizi zilizonza mapema mwaka 2013 zitahusiaha ngazi ya taifa na majimbo nchini Pakistan na ukuzaji wa lishe unatarajiwa kujumuisha wadau na sekta mtambuka za taifa hilo.

Takwimu za shirika hilo zinaonyesha kuwa watoto wawili kati ya watano ambao ni asilimia 44 wamedumaa, kutokana na unyafuzi, hali ambayo ina madhara ya muda mrefu kwa maendeleo yao ya kimwili na kiaikili.