Tekelezeni ahadi ya amani kama mlivyokubaliana:Ban

17 Oktoba 2016

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini umeripoti hali ya utulivu katika eneo la Malakal nchini humo, lakini bado kuna mvutano baada ya mapigano ya Ijumaa baina ya jeshi la serikali la SPLA na lile la SPLA upinzani.

Sambamba na hilo, UNMISS imesema wakimbizi wa ndani 67 wamewasili katika jengo la ujumbe huo kutafuta hifadhi kufuatia mlipuko uliotokea katika jimbo la Unity.

Ujumbe huo pia imesema una wasiwasi mkubwa na kuendelea kwa mapigano baina ya majeshi hayo mawili na kuleta mateso kwa wananchi.

Katika ujumbe wake kupitia kwa msemaji wake Stephan Dujarric, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema..

(Sauti ya Stephan)

"Natoa wito kwa wadau wa mzozo kuheshimu ahadi ya kusitisha mapigano, ahadi iliyokubaliwa na pande hizo mbili Julai, na nasisitiza haja ya kutelekeza makubaliano ya amani."

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter