Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila nchi ipinge usafirishaji haramu wa binadamu:UNODC

Kila nchi ipinge usafirishaji haramu wa binadamu:UNODC

Yury Fedotov , mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC, leo Jumatatu ametoa wito kwa nchi zote duniani kujiunga na vita dhidi ya wasafirishaji haramu wa binadamu, waingizaji kinyemela wahamiaji na kutekeleza mkataba wa Umoja wa mataifa kuhusu uhalifu wa kupangwa kimataifa(UNTOC).

Akizungumza katika tukio maalumu kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu, Bwana Fedotov amesema anazitaka nchi kuchukua hatua kwa muda mfupi, na kwa kufanya hivyo watakuwa wanasaidia mapambano dhidi ya waingizaji kinyemela na wasafirishaji haramu wa watu.

Bwana. Fedotov amelipongeza azimio la New York kuhusu wakimbizi na wahamiaji akisema lina vipengee muhimu katika utekelezaji wa UNTOC.

Kwa mujibu wa utafiti wa UNODC, asilimia 79 ya wahanga wa usafirishaji haramu ni wanawake na watoto na wengi wao ni wahamiaji. Ofisi hiyo itataka vitendo hivyo vikomeshwe na kuhakikisha wahusika hawakwepi tena sheria.