Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Binti mfalme wa Thai kuiwakilisha FAO katika utokomezaji njaa

Binti mfalme wa Thai kuiwakilisha FAO katika utokomezaji njaa

Shirika la chakula na kilimo FAO leo Jumatatu limetangaza kwamba Binti mfalme Maha Chakri Sirindhorn wa Thailand,amekubali kuwa kuliwakilisha shirika la FAO kama balozi mwema wa kutokomeza njaa.

Tangazo hilo limetolewa wakati wa maadhimisho ya 36 ya siku ya chakula duniani kwenye ofisi ya kanda ya Asia na Pacific ya shirika hilo mjini Bangkok.

Kufikia lengo la kuwa na njaa surufi duniani ifikapo mwaka 2030 ni moja ya malengo ya maendeleo endelevu (SDG 2) yaliyoandaliwa na kukubaliwa na jumuiya ya kimataifa. FAO imetajwa kuwa ni shirika mlezi wa lengo hilo nambari 2 la kutokomeza njaa.

Na limesema kukubali kwa binti mfalme huyo kuwa balozi mwema wa kutasaidia sana katika kuelimisha kuhusu sera na umma hasa nini cha kufanya kwa pamoja kuhakikisha dunia bila njaa inakuwa sio ndoto tena.