Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yachangia dola milioni 60 kwa uchumi wa Uganda

WFP yachangia dola milioni 60 kwa uchumi wa Uganda

Shirika la Mpango wa Chakula,WFP limechangia karibu dola milioni sitini kwa uchumi wa Uganda kupitia ununuzi wa chakula na ujenzi wa maghala ya chakula nchini humo. Taarifa kamili ja John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

WFP imesema, imenunua tani za nafaka zaidi ya 97,000 zenye thamani ya dola milioni 36 mnamo mwaka huu pekee kwa ajili ya kusaidia maelfu ya wakimbizi na wananchi wakiwemo watoto wanaokabiliwa na utapiamlo.

Pia limetoa dola milioni 14 kwa makampuni ya usafirishaji Zaidi ya 41, huku dola milioni 7.8 zikitumiwa katika ujenzi wa maghala ya chakula ya Tororo na Kampala pamoja na maghala mengine 12 kote nchini.

Mike Sackett, Khaim Mkurugenzi wa WFP, Uganda amesema, chakula kilichonunuliwa humo nchini kimekuwa kikitumiwa kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa waliokatika uhitaji katika kanda nzima wakiwemo wale nchini Sudan Kusini na Ethiopia