Pande hasimu Iraq zizingatie sheria za kimataifa za binadamu: O’Brien

Pande hasimu Iraq zizingatie sheria za kimataifa za binadamu: O’Brien

Mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Stephen O’Brien amesema anahofia usalama wa watu takriban milioni 1.5 wanaoishi Mosul Iraq, ambao huenda wakaathirika vibaya na operesheni za kijeshi za kurejesha udhibiti wa mji huo mikoni mwa serikali kutoka kwa kundi la ISIL.Assumpta Massoi na taarifa kamili

(STAARIFA YAASSUMPTA)

O'Brien amesema familia ziko katika hatari kubwa ya kukumbwa na mashambulizi kutoka kwa walenga shabaha . Maelfu ya wasichana na wavulana , wanawake na wanaume wanaweza kuzingirwa au kutumiwa kama ngao vitani, huku wengine kwa maelfu wakifungishwa virago kwa lazima au kukwama katikati ya mapigano.

Amerejea wito wake kwa pande zote kwenye mzozo huo kutimiza wajibu wao chini ya sheria za kibinadamu za kimataifa, na kuhakikisha watu wanapata fursa ya msaada wanaostahili.

Ameongeza kuwa malazi hivi sasa yapo tayarui kwa ajili ya watu 60,000 kwenye kambi na ujenzi wa makazi mengine unaendelea ili kuweza kuhifadhi watu 250,000. Pia chakula kwa zaidi ya watu laki mbili kipo tayari.