Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilimo kina fursa kubwa katika upunguzaji wa gesi chafuzi:FAO

Kilimo kina fursa kubwa katika upunguzaji wa gesi chafuzi:FAO

Ahadi ya kutokomeza njaa lazima iende sanjari na mabadiliko ya haraka ya kilimo na mifumo ya chakula ili kuhimili hali ya hewa inayobadilika, imesema leo ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo duniani,FAO.

Kilimo, kikijumuisha masuala ya misitu, uvuvi na ufugaji kinazalisha takribani 1/5 ya gesi chaguzi duniani. Ripoti hiyo "Hali ya chakula na kilimo 2016” inasema kilimo ni lazima kichangie zaidi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi huku kikijitahidi kudhibiti athari zake.

Kwa mujibu wa Jose Graziano da Silva mkurugenzi mkuu wa FAO, hakuna shaka kwamba mabadiliko ya tabianchi yanaathiri uhakika wa chakula, na hakuna atakayeweza kuhakikisha kwamba tutavuna tulichopanda kutokana na hali hiyo ya sintofahamu, hali inayochangia kupanda kwa bei ya chakula pia.