Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa makazi duniani HABITAT III waanza leo Quito, Ecuador

Mkutano wa makazi duniani HABITAT III waanza leo Quito, Ecuador

Mkutano wa tatu wa makazi duniani, HABITAT III unaanza hii leo huko Quito, Ecuador, lengo ikiwa ni kupitisha ajenda mpya ya miji.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la makazi duniani, HABITAT, Joan Clos amesema mkutano huko wa Nne, utaibuka na nyaraka yenye lengo la kuboresha makazi mijini, ili hatimaye kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

HABITAT inasema asilimia 55 ya wakazi wa dunia hivi sasa wanaishi mijini, idadi ambayo inatarajiwa kuongezeka maradufu ifikapo mwaka 2050.

Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ni Rachel Kamweru, mwakilishi kutoka bunge la kaunti ya Nairobi, nchini Kenya ambaye ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa huko Quito kuwa matarajio yake ni,,

(Sauti ya Rachel)

Amesema ana matumaini makubwa na mkutano huo kwa kuwa umejumuisha washiriki kutoka mashinani na kwamba

(Sauti ya Rachel)