Skip to main content

Ban ashuhudia uharibifu wa kimbunga Matthew na kusema hali ni tete: Ban

Ban ashuhudia uharibifu wa kimbunga Matthew na kusema hali ni tete: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametembelea Haiti kujionea uharibifu uliosababishwa na kimbunga Mathew kilichoipiga nchi hiyo zaidi ya juma moja lililopita.

Ban ametumia ndege kuruka katika eneo liitwalo Les Cayes ili kujionea kutoka ngani uharibifu, na baada ya kushuhudia hali ilivyo akasema hali ni tete na hivyo kutaka wale aliowaita marafiki wa Haiti kusaidia taifa hilo.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, karibu watu milioni moja na nusu wameathiriwa na kimbunga Mathew, huku zaidi ya laki tatu na nusu wakihitaji msaada wa kibinadamu.

Katibu Mkuu amesema baada ya kuwaona watu waliopoteza kila kitu, alielewa maumivu na hasira zao.

Juma lililopita Umoja wa Mataifa ulizindua ombi la dola milioni 120 kusaidia kukidhi mahitaji yanayotolewa na Umoja wa Mataifa katika kipindi cha meizi mitatu ijayo.