Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chakula na kilimo viende sanjari na mabadiliko ya tabia nchi:FAO

Chakula na kilimo viende sanjari na mabadiliko ya tabia nchi:FAO

Hali ya hewa duniani inabadilika, hivyo uzalishaji wa chakula na kilimo lazima vibadilike pia kwenda sanjari na mabadiliko hayo. Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO katika maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 16.

Bwana Da Silva amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni hali ya hewa inabadilika ,na hivyo ametoa wito kwa nchi kujumuisha masuala ya chakula na kilimo katika mipango ya hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Ameongeza kuwa uwekezaji hasa katika maeneo ya vijijini ni muhimu sana ili kuhakikisha uhakika wa chakula

(SAUTI YA GRAZIANO)

“Chakula ni haki ya msingi ya binadamu , lakini bado kuna watu karibu milioni 800 wanakabiliwa na njaa duniani kote, bila uhakika wa chakula na na l ibe ya kutosha kwa wote malengo ya maendeleo endelevu hayawezi kufikiwa , ndio maana ajenda yam waka 2030 intoa wito wa kutokomeza njaa pamoja na kuchagiza kilimo endelevu”

image
Bwana Da Silva amesisitiza kuwa chakula ni haki ya msingi ya binadamu. Picha: FAO/Daniel Hayduk
Hata hivyo akaonya kuwa

(SAUTI YA GRAZIANO)

“Malengo haya ni bayana yako hatarini wakati mabadiliko ya hali ya hewa yakiendelea, tayari yanaathiri rutuba kwenye udongo, misitu, bahari, maeneo ambayo ni tegemeo kwa sekta ya kilimo na uhakika wa chakula.wahanga wakubwa ni wakulima wadogowadogo wanaoishi katika maeneo ya vijijini kwenye nchi zinazoendelea , hawana nyezo za kukabiliana na mabadiliko ya htabia nchi”

Ameongeza na ndio maana

(SAUTI YA GRAZIANO)

“Siku ya chakula duniani mwaka huu  inatanabaisha kwamba hali ya hewa inabadilika , na chakula na kilimo ni lazima vibadilike pia.”