Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kauli ya msichana mwenye ndoto ni moto yathibitika UM

Kauli ya msichana mwenye ndoto ni moto yathibitika UM

Mtoto wa kike! Ni lulu ambayo kila inapotaka kung’ara hukumbwa na utando wa kuikwamisha. Harakati za kuzuia kung’ara kwa kundi hilo kumesababisha watoto zaidi ya milioni 62 kote ulimwenguni kutokwenda shule. Sababu kama vile mila na desturi potofu, vita na hata ukata zinatajwa. Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia hilo, miaka mitano iliyopita ilitenga tarehe 11 mwezi Oktoba ya kila mwaka kuwa siku ya mtoto duniani. Katika maadhimisho ya mwaka huu, ngonjera zilishika kasi kuonyesha madhila na ndoto za mtoto wa kike, shuhuda wetu ni Brian Lehandar.