Neno la wiki - Pakubwa

14 Oktoba 2016

Katika Neno la Wiki hii  Oktoba 14 tunaangazia neno pakubwa na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, huko nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema katika mazungumzo,  watu wengi  wamekuwa wakitumia kiwakilishi cha mahali kwa maana ya "pa"..pahali pale au pakubwa au padogo kwa maana ya kuonyesha kwamba kile kinachokizungumzia  kinakusudia kuonyesha mahali au kitu kinachokizungumzia kuonyesha  uwezo wake.  Katika matumizi ya kawaida ya lugha ya kiswahili, tunaweza kutumia neno hilo ili  kuleta upatanisho  wa kisarufi vizuri. lakini pia, neno hili limekuwa likitumika zaidi kutokana na lahaja ambayo baadhi ya watu katika matumizi  yao hutumia neno "pa" kama kiwakilishi cha mahali. Ili liweze kuleta maana nzuri ni lazima liwe linazingatia au linaonyesha mahali. Kwa mfano.."watu wengi hupenda kununua pahala pakubwa kwa ajili ya kujenga nyumba".

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter