Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna haki ya kuwaua watoto: UNICEF

Hakuna haki ya kuwaua watoto: UNICEF

Hakuna kinachohalalisha kuwaua watoto, hii ni kwa kauli ya mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Syria, Bi Hanaa Singer aliyoitoa kufuatia vifo vya watoto wanne mjini Allepo hapo jana.

Ripoti zinasema kuwa watoto wengine watatu wamejeruhiwa baada ya UNICEF kuvurumishiwa bomu kulipuka wakati wakiwa njiani kuelekea shuleni asubuhi.

UNICEF inasema mauaji hayo yamefanyika siku tatu baada ya watoto wengine kuuliwa wakiwa ndani ya shule mjini Dara’a ishara kwamba nchini Syria sasa hata kwenda shule ni kuhatarisha maisha.

Bi Singer akilaani vitendo hivyo amenukuliwa akisema katika mji wa Aleppo kila siku mashambulizi yanatokea bila kubagua dhidi ya maeneo yaliyo na wakazi wengi na zaidi kuwaua watoto.