Watoto watano kati ya sita hawapati lishe muafaka: UNICEF
Umempa lishe ya kutosha leo mwanao? Sikia habari hii, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema watoto watano kati ya sita walioko chini ya umri wa miaka miwili, hayalishwi ipasavyo vyakula vyenye virutubisho mujarabu kwa umri wao. Rosemary Musumba na taarifa zaidi.
( TAARIFA YA ROSE)
Kwa mujibu wa ripoti ya mpya ya UNICEF, ukosefu wa virutubisho hivyo unawanyima nguvu na virutubishio wanavyohitaji katika muda muhimu kwa ajiali ya maendeleo yao ya kimwili na utambuzi.
France Begin ambaye ni mshauri wa lishe katika UNICEF anasema watoto wakiamo wachanga, wana uhitaji mkubwa wa virutubisho kuliko wakati wowote ule wa maisha yao lakini la kusikitisha ni kwamba miili na ubongo wa wa mamilioni ya watoto hawatimizi haja hiyo kwani wanapata chakula kidogo au kwa kuchelewa.
Amesema lishe duni katika umri mdogo inasababisha kudumaa akili kusikorekebishika na uharibifu wa kimwili.