Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yataka uchunguzi wa haraka wa kifo cha mwandishi wa habari Sudan Kusini

UNESCO yataka uchunguzi wa haraka wa kifo cha mwandishi wa habari Sudan Kusini

Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, Irina Bokova amelaani vikali mauaji ya mwandishi habari mkongwe wa kujitegemea Isaac Vuni, yaliyotokea katika eneo la Kerepi, Sudan Kusini mnamo tarehe 26 Septemba.

Bi. Bokova ametoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini, kuchunguza mauaji ya mwandishi habari huyo na kuwaleta mbele ya sheria wale wanaotumia ukatili kunyamazisha vyombo vya habari na kuwanyima watu haki yao huru ya msingi ya kupata habari, akisema hatua hiyo ni muhimu katika jamii kwa ujumla.

Mkuu huyo ametoa wito huu sambamba na kupitishwa kwa azimio nambari 29 linaloitwa "Hukumu ya Ukatili dhidi ya Waandishi wa Habari", azimio lililopitishwa na nchi wanachama wa UNESCO.