Ban ahuzunishwa na kifo cha mfalme Bhumibol Adulyadej wa Thailand

Ban ahuzunishwa na kifo cha mfalme Bhumibol Adulyadej wa Thailand

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya kifalme, serikali na watu wa Thailand kufuatia kifo cha mfalme Bhumibol Adulyadej. Katibu mkuu anatambua huduma ya muda mrefu ya mfalme Bhumibol kwa taifa lake, lakini pia kumbukumbu aliyoiacha kama kiongozi kiungo wa kitaifa.

Mfalme huyo alihudusiwa na kuheshimiwa na watu wa Thailand lakini kimataifa pia. Kwa kutambua kazi zake alienziwa na shirika na Umoja wa mataifa la mpango wa maendeleo UNDP kwa kutunukiwa tuzo ya maisha mwaka 2006.

Katibu Mkuu ameelezea matumaini kwamba Thailand itaendelea kumuenzi mfalme huyo kwa kurithi na kuendeleza azma yake ya maadili ya kimataifa na kuheshimu haki za binadamu na demokrasia.