Guterres Katibu Mkuu mteule wa Umoja wa Mataifa.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limemuidhinisha Antonio Guterres wa Ureno kuwa Katibu Mkuu wa Tisa wa chombo hicho chenye nchi wanachama 193. Assumpta Massoi na ripoti kamili.
(Taarifa ya Assumpta)
Nats..
Ndani ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Baraza hilo Peter Thomson akiitisha kikao cha kumuidhinisha Antonio Guterres wa Ureno kuwa Katibu Mkuu wa chombo hicho.
Nats..
Rais wa Baraza la Usalama Balozi Vitaly Churkin akasoma pendekezo lao..
Rais wa Baraza Peter Thomson akawasilisha rasimu ya pendekezo la kumuidhinisha Guterres…. Mwitikio..
Nats..
Baraza limempitisha kwa kauli moja..Guterres akatokea mbele ya wanachama..
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anayemaliza muda wake Ban Ki-moon ameanza hotuba yake kwa pongezi kwa Katibu Mkuu mteule, Guterres.. na zaidi ya yote kwa nchi wanachama, akisema si kwa chaguo lao tu, bali pia kwa jinsi walivyoendesha mchakato mzima wa kumpata.
“Katibu Mkuu mteule Guterres anafahamika vyema miongoni mwetu humu ukumbini. Lakini pengine anafahamika zaidi kule kwenye mahitaji; kule kwenye mizozo na machungu ya kibinadamu.”
Na ndipo Guterres akapanda jukwaani..
(Sauti ya Guterres)