Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazingira sasa yanavutia wawekezaji kwenye miundombinu Afrika- NEPAD

Mazingira sasa yanavutia wawekezaji kwenye miundombinu Afrika- NEPAD

Afisa Mtendaji Mkuu wa mpango mpya kwa maendeleo ya Afrika, Dkt. Ibrahim Mayaki amesema nuru ya uwekezaji katika sekta ya miundombinu barani Afrika sasa inan’gara kwa kuwa mambo ya msingi yanayovutia wawekezaji yameanza kushughulikiwa.

Amesema hayo jijini New York, Marekani akihojiwa na Jocelyn Sambira wa Radio ya Umoja wa Mataifa ambapo ametaja mambo hayo kuwa ni..

(Sauti ya Mayaki)

 “Masuala ya kanuni za udhibiti, kuhuisha mifumo ya udhibiti, tumeshatatua suala la vipaumbele vya miradi na kuwa na uungwaji mkono kisiasa na sasa tunaelekea katika kukamilisha suala la kupatia fedha miradi hiyo.”

Bwana Mayaki ambaye anahudhuria wiki ya Afrika ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na

 (Sauti ya Mayaki)

 “Bwawa la Sambangalou huko Afrika Magharibi la kuzalisha nishati ya umeme, bomba la kusafirisha gasi kutoka Nigeria kupitia Niger hadi Algeria,ambalo linaendelea vizuri,   na mradi wa ukanda wa kati au LAPSSET kutoka eneolaBurundi kwenda Dar es salaam na mradi wa ukanda wa Kaskazini hadi Kusini  Afrika.”

 Amesema mpango wa NEPAD wa uendelezaji wa miundombinu Afrika, PIDA umerahisisha uwekezaji na  kwamba miradi  hiyo imewezekana baada ya ..

 (Sauti ya Mayaki)

 "Kuweza kuwashawishi wawekezaji kwa msingi wa mifano halisi. Lakini kwa misingi ya utawala bora katika nchi ambako tunaenda kuwekeza kumewezesha wapate faida ambayo wasingaliweza kupata katika nchi nyingine duniani.”