Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukuaji wa miji una faida kubwa lakini pia hatari:UN-HABITAT

Ukuaji wa miji una faida kubwa lakini pia hatari:UN-HABITAT

Mchakato wa ukuaji wa miji una faida lakini vilevile hatari kubwa, kwa mujibu wa afisa wa Umoja wa Mataifa atakeongoza mkutano wa kimataifa kuhusu mustakhbali wa miji duniani kwa miaka 20 ijayo.

Mkutano wa tatu wa makazi (HABITAT 111) kama unavyojulikana utaanza rasmi mwishoni mwa wiki hii mjini Quito nchini Ecuador, na utahudhuriwa na maelfu ya watu, na wawakilishi kutoka kila pembe ya dunia ili kupitisha ajenda mpya ya mipango miji.

Ajenda hiyo itaweka viwango vipya vya kimataifa kwa ajili ya ukuaji endelevu wa majiji na miji.

Katibu Mkuu wa mkutano huo na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT, ni Joan Clos.

Akiwa njiani kuelekea Quito amezungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu mkutano huo..

(SAUTI JOAN CLOS)

“Ukuaji wa miji una faida kubwa lakini pia una hatari kubwa, ajenda mpya ya ukuaji wa miji ni mapendekezo ya kupitia upya ukuaji wa miji na kuepuka makossa yaliyokuwa yakitokea kwa miaka 20 iliyopita. Tukiangalia takwimu wakati huohuo ambapo ukuaji wa miji ulikuwa unaongezeka , ubora wa miapango miji ulikuwa unashuka , na hilo limesababisha hali mbaya sana”