Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia Haiti wahitaji usaidizi baada ya kimbunga

Raia Haiti wahitaji usaidizi baada ya kimbunga

Umoja wa Mataifa unasema Haiti ambayo juma lililopita ilikumbwa na kimbunga Mathew inakabiliwa na magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu na hivyo hatua zaidi za usaidizi zinahitajika.

Zaidi ya watu milioni moja wameathiriwa na kimbunga hicho na juma hili umoja huo ulichukua hatua katika kusongesha usaidizi. Ungana na Joseph Msami katika makala inayoeleza hali halisi nchini Haiti baada ya janga hilo.