Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lishe duni inaathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa Chad:WFP

Lishe duni inaathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa Chad:WFP

Uchumi wa Chad unapoteza jumla ya Chad Franc bilioni 575.8 sawa na dola za Marekani billion 1.2 kwa mwaka au asilimia 9.5 ya pato la taifa kutokana na athari za lishe dunia kwa watoto, imesema ripoti ya utafiti mpya iliozinduliwa leo mjini Djamena.

Ripoti hiyo “Gharama za njaa barani Afrika: Athari za muda mrefu za kiuchumi na kijamii za lishe duni kwa watoto Chad “(COHA), inaonyesha kwamba fedha nyingi zinpotea kutokana na ongezeko la gharama za huduma za afya, mzigo aidi wa mfumo wa elimu na uzalishaji mdogo wa wafanyakazi.

Utafiti unaonyesha kwamba asilimia 56.4 ya watu wazima walikabiliwa na maradhi ya kudumaa walipokuwa watoto, na hii inawakilisha zaidi ya watu milioni 3.4 ya nguvu kazi ya taifa hilo ambayo haiwezi kufikia kilele cha uwezo wao wa kufanya kazi kutokana na athari za lishe duni utotoni.

Uwezo mdogo wa kimwili katika uzalishaji unalipotezea taifa la Chad Chad Franc bilioni 63.7 kwa mwaka kutokana na maradhi yenye uhusiano na lishe dunia ya utotoni , huku maradhi hayo yakigharimu Chad Franc zingine bilioni 168.5 kwa matibabu.