Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miji ya baadaye lazima izingatia utamaduni na sayansi, UNESCO yatetea katika mkutano wa Habitat III

Miji ya baadaye lazima izingatia utamaduni na sayansi, UNESCO yatetea katika mkutano wa Habitat III

Uzito wa Utamaduni katika maendeleo endelevu ya mijini na masuala ya maji katika miji mikubwa ni jukumu kubwa katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi. Hizo ni miongoni mwa mada za shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO zitakazojadiliwa kwenye mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu makazi na maendeleo endelevu ya mijini (Habitat III), utakaofanyika mjini Quito, Ecuador, 17-20 Oktoba.

Takwimu kutoka shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa makazi UN-Habitat zinaeleza kuwa miji milioni moja itakuwa na takriban watu bilioni 3.9 ambayo ni zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani. Kwa mwenendo huo inakadiriwa kuwa kufikia mwaka 2050, theluthi mbili ya wakazi wa sayari watakuwa wakiishi mijini.

Masuala mengine yatakayojadiliwa ni kama vile usimamizi wa mahitaji ya miji, bei ya maji au usafi wa mazingira, kukuza ushirikishwaji na kutobaguliwa katika maeneo ya mijini. Wakuu wa serikali, mawaziri 150 wanaosimamia masuala ya makazi , mamia ya mameya wa miji ikiwa ni pamoja na wa Paris (Ufaransa), Bogota (Colombia) na Johannesburg (Afrika Kusini), wawakilishi wa kitaifa, mitaa na mashirika ya kiraia watashiriki katika mkutano huo, ili kupitisha ajenda mpya kwa ajili ya miji, kwa miaka ishirini ijayo.

Na kwa uzinduzi wa ripoti hiyo ambayo ni ya kwanza inayoangazia mambo ya utamaduni, UNESCO itaonyesha jukumu la kimkakati la utamaduni kupitia urithi, na uzito wa viwanda bunifu ili kufikia mafanikio ya maendeleo endelevu ya mijini.

Mkutano wa masuala ya makazi na maendeleo ya mijini unafanyika kila baada ya miaka ishirini , wa hapo awali ulifanyika mjini Vancouver, Canada mwaka wa 1976 na Istanbul, Uturuki mwaka wa 1996.