Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha tangazo la kuanza majadiliano Colombia baiana ya serikali na ELN

Ban akaribisha tangazo la kuanza majadiliano Colombia baiana ya serikali na ELN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tangazo kwamba serikali ya Colombia na jeshi la ukombozi la taifa ELN wataanza majadiliano rasmi Oktoba 27 mjini Quito, Ecuador.

Mazungumzo hayo yataanza baada ya zaidi ya miaka miwili ya utoaji maelezo. Ban amesema huu ni mwanzo wa kuwatia moyo wananchi wa Colombia na wale wote wanaounga mkono kumalizika kwa amani kwa mgogoro uliodumu kwa miongo kadhaa nchini humo.

Katibu Mkuu anatarajia kwamba serikali ya Colombia na ELN watafanya kila wawezalo kuhakikisha wanafikia makubaliano ya amani endelevu haraka iwezekanavyo. Amezipongeza serikali za Brazil, Chile, Cuba, Ecuador, Norway na Venezuela kwa kuchangia katika mchakato huo.