Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yafunga virago Burundi

Ofisi ya haki za binadamu yafunga virago Burundi

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imefungasha virago vyake nchini Burundi baada ya kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 20. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Ofisi hiyo inasema hatua hiyo imefikiwa baada ya serikali Burundi baada ya kuamua kutotoa ushirikiano tena. Akizungumzia hatua hiyo msemaji wa ofisi hiyo Cecile Pouily amesema

(SAUTI YA POULILY)

“Bila shaka tunatiwa wasiwasi na uamuzi wa serikali ya Burundi kuamua kusitisha ushirikiano wa aina yoyote na ofisi yetu, tumefanya kazi humo kwa miaka mingi mkataba nan chi hiyo ulianza Novemba 1995, na tunadhani kazi tuliyokuwa tunafanya ni ya muhimu sana na iliyozaa matunda”

Ameongeza kuwa ingawa ofisi hiyo imejitahidi na kufanikisha masuala mengi lakini sasa ni mapema kujua mustakhbali wao Burundi

(SAUTI YA POUILY )

“Burundi hivi sasa iko katika wakati muhimu sana , na ni muhimu majadiliano kuhusu hali ya haki za binadamu yanaendelea , serikali ya Burundi imesema inataka kuzungumza nasi kuhusu mustakhbali wa ofisi yetu na sasa ni mapema mno kusema lolote kwani lazima uamuzi ufanyike”