Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali Sudan Kusini ni ya kutia wasiwasi-UM

Hali Sudan Kusini ni ya kutia wasiwasi-UM

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini una wasiwasi mkubwa juu ya kuongezeka kwa migogoro yenye kutumia silaha katika maeneo mbali mbali nchini humo yaliyoanza wiki chache zilizopita.Taarifa kamili na Amina Hassan.

(TAARIFA YA AMINA)

UNMISS imesema, mapigano yenye kutumia silaha kali baina ya makundi ya SPLA na SPLA pinzani yanafanyika katika mji wa Leer na kusababisha vifo vya raia na kuwafungisha virago wengine wengi wanaokimbilia vichakani na katika maeneo yaliyojaa maji.

Vile vile kumeripotiwa vifo vya raia zaidi ya 20 katika maeneo ya Equatoria vilivyosababishwa na kundi lisilojulikana, wakiwemo wanawake na watoto, na raia wengine watano kufariki baada ya jeshi la serikali kurejesha mashambulizi.

Wakati huo huo, UNMISS imesema inaendelea kuwasiliana na serikali na makundi ya SPLA kuondoa vikwazo dhidi ya ujumbe huo kuingia maeneo yenye migogoro kufanya tathmini, na inatoa wito kwa wadau wa mzozo kusitisha haraka mapigano nchini humo, na kuwakumbusha kuwa mashambulizi hayo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.