Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yapokea dola zaidi ya milioni 2 toka Japan kuboresha lishe Uganda

WFP yapokea dola zaidi ya milioni 2 toka Japan kuboresha lishe Uganda

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, nchini Uganda limekaribisha mchango wa dola milioni mbili nukta tano kutoka kwa serikali ya Japani ili kulisaidia kuboresha lishe miongoni mwa watu katika eneo la Karamoja Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Taarifa kamili na John Kibego.

(TAARIFA YA KIBEGO)

Kaimu mkurugenzi wa WFP, Uganda, Mike Sackett, ameonyesha matumaini kuwa, mchango huo utasaidia kuimarisha lishe miongoni mwa watoto, akinamama na wajawazito wapatao 50,000 katika eno lililomaskini Zaidi la Karamoja.

Bwan Sacket ameomgezea kuwa watatumia fedha hizo kununua tani 1,700 za chakula maalumu, sukari, na mafuta kwa watoto walio kati ya umri wa miezi sita na miezi ishirini na mitatu, ili kuwazuia kudumaa.

Zaidi ya 39.5% ya watoto wadogo katika eno la Karamoja wamedumaa kutokana na lishe duni huku serikali ya Uganda ikiwa inalazimika kutoa 5.6 % ya mapato yake ya ndani kila mwaka kwa ajili ya kusimamia lishe miongoni mwa watoto wanaokabiliwa na utapiamlo.