Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chonde chonde ongezeni muda wa MINUSTAH ili kuimarisha usaidizi

Chonde chonde ongezeni muda wa MINUSTAH ili kuimarisha usaidizi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao kuhusu Haiti ambapo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Sandra Honore amesema kimbunga Matthew kimeongeza machungu ambayo tayari wananchi walikuwa wanakumbana nayo.

Akihutubia kwa njia ya video kutoka Port au Prince, Bi. Honore amesema maeneo ya kusini, hali ni mbaya kwani hata mazao yamesombwa, miundombinu imesambaratishwa, huku mchakato wa kisiasa ikiwemo chaguzi zimeahirishwa.

Kwa mantiki hiyo, Bi. Honore ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, MINUSTAH amesema..

(Sauti ya Bi. Honore)

“Athari za kimbunga Matthew kwenye mchakato wa siasa na utulivu wan chi unaweza kuwa kigezo cha msingi cha kuthibitisha pendekezo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kuongeza kwa miezi sita hadi tarehe 15 Aprili mwaka 2017 muda wa MINUSTAH, ikiwa na kiwango cha sasa cha polisi na askari. Hatua hii itawezesha MINUSTAH kusaidia jitihada za mamlaka za Haiti za kurejesha katika utulivu wa kikatiba wakati huu wa janga la kibinadamu lililosababishwa na kimbunga Matthew.”

Awali muda wa MINUSTAH ulikuwa umalizike tarehe 15 mwezi huu wa Oktoba.