Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuimarisha ukusanyaji takwimu ni muhimu katika kutatua matatizo ya kijinsia

Kuimarisha ukusanyaji takwimu ni muhimu katika kutatua matatizo ya kijinsia

Kuboresha ukusanyaji wa takwimu kuhusu masuala yanayowakabili wasichana kote duniani kutatoa mwangaza wa maisha yao na kuwasaidia kutatua matatizo yao, kwa mujibu wa shirika la umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA.

Takwimu zinaweza kutumika kuimarisha na kupanua wigo wa usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake, masuala ambayo ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDG’s.

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya mtoto wa kike, satvika Chalasani msemaji wa UNFPA anafafanua changamoto zinazowakabili wasichana hasa vigori

(SAUTI YA CHALASANI)

Ndoa za utotoni na za lazima, idadi kubwa ya vifo vitokanavyo na mimba zisizotarajiwa, kiwango kikubwa cha maambukizi ya HIV, na kuna kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia ambao wasichana na wanawake wanakabiliwa nao kote duniani”