Skip to main content

Hali tete DRC yakwamisha uchaguzi wa amani: MONUSCO

Hali tete DRC yakwamisha uchaguzi wa amani: MONUSCO

Hali ya kisiasa sio shwari nchini Jamhuri ya Kidemokrsia ya Kongo DRC, hatua inayozuia mchakato wa uchaguzi wa amani na majadiliano kuendelea amesema Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo Maman Sidikou. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa mjini New York ambapo hii leo baraza la usalama linajadili hali nchini DRC, Bwana Sidikou amesema mkwamo wa uchaguzi wa Rais na kuwekwa korokoroni kwa baadhi ya wafuasi wa upinzani ni miongoni mwa sababu ya hali tete nchini humo.

Wakati hayo yakiendelea kambi kuu ya upinzani imesusia majadiliano yanaoyoongozwa na Muungano wa Afrika AU, yaliyozinduliwa mwezi Septemba. Mkuu huyo wa MONUSCO anasema.

( SAUTI SIDIKOU)

‘‘Inasikitisha sana kwa kuwa tulitarajia uchaguzi wa amani DRC kwa mara ya kwanza, hakika tunahitaji kujua nini kimetokea, nani kafanya nini na vikwazo vitumike.’’