Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake washirikishwe zaidi kwenye uchaguzi ujao Somalia

Wanawake washirikishwe zaidi kwenye uchaguzi ujao Somalia

Jumuiya ya kimataifa imesema inatambua uteuzi wa majina ya wagombea katika bunge la shirikisho nchini Somalia, uliofanyika Oktoba 8 na 9

Wadau hao Umoja wa mataifa, Muungano wa Afrika, Ethiopia, Muungano wa Ulaya, IGAD, Italy, Sweden, Uingereza na Marekani wamesema wanakaribisha msimamo huo wa timu ya shirikisho ya utekelezaji wa masuala ya uchaguzi (FIEIT) , ambayo imesisitiza haja ya kutimiza sheria na taratibu za mchakato wa uchaguzi, maamuzi na nia  ya viongozi wa Somalia waliyoiweka bayana.

Pia jumuiya ya kimataifa imekaribisha kutengwa kwa viti viwili kwa ajili ya wanawake Kusini Magharibi , kupitia uchaguzi wa wanawake pekee.

Pia wamesema wanaunga mkono wito wa timu hiyo wa kutathimini majina ya wagombea katika saa 48 katika majimbo ya Galmudug, Jubbaland and Puntland, sanjari na utaratibu uliokubaliwa na kongamano la kitaifa la uongozi.

Na muda huo wa saa 48 ni lazima uzingatiwe ili majimbo wanachama wa shirikisho kuwachagua wabunge wao wa bunge kuu bila kuchelewa.