Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubia wa maendeleo na amani vyamulikwa katika wiki ya Afrika

Ubia wa maendeleo na amani vyamulikwa katika wiki ya Afrika

Wiki ya Afrika katika Umoja wa Mataifa imeanza leo ikiwa na maudhui ya kuimarisha ubia kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu SGDS, utawala bora, amani na utulivu barani Afrika. Amina Hassan na maelezo zaidi.

( TAARIFAYA AMINA)

Katika mkutano wa ufunguzi wa wiki ya Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema juhudi zaidi za utatuzi wa migogoro katika ukanda wan chi za maziwa makuu, ukanda wa Sahel, na maeneo mengine zinahitajika ili kuwezesha maendeleo barani humo.

Kuhusu hali ya kisiasa Katibu Mkuu amesema utawala bora umeimarika barani Afrika lakini bado kuna changamoto.

( SAUTI BAN)

‘‘Wakati idadi kubwa ya nchi za Afrika zimeandaa uchaguzi wa vyama vingi, baadhi ya matukio ya ukosefu wa uaminifu yamezitumbukiza katika migogoro. Pia tumeshuhudia juhudi za kutoheshimu demokrasia ikiwamo viongozi kuzidisha muda wa utawala kwa mujibu wa katiba.’’

Akizungumza na idhaa hii muda mfupi kabla ya mkutano huo kaimu mwenyekiti wa kamisheni ya Muungano wa Afrika AU Erastus Mwencha amesema ili kufanikisha ajenda ya Afrika ya 2063 bara hilo linapaswa.

( SAUTI MWENCHA)