Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yatoa wito wa kusitishwa uhasama mara moja Yei

UNMISS yatoa wito wa kusitishwa uhasama mara moja Yei

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umesema unatiwa hofu na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama kwenye mji wa Yei ambapo UMNISS imeendelea kunyimwa fursa ya kufika na kutathimini hali halisi na madhila yanayowakabilia maelfu ya watu wanahitaji msaada.Yasmina Bouziane afisa habari wa mpango huo

(SAUTI YA YASMINA )

“Yote haya yameathiri zaidi ya Wasudan Kusini 100,000 katika eneo la Yei, hasa ukizingatia kwamba kuna raia wasio wapiganaji ni bughuda tupu”

Ameongeza kuwa UNMISS imepokea taarifa za kutisha za ukatili unaoendeshwa dhidi ya raia wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto. Imetoa wito kwa pande zote kusitisha uhasama na kutoa fursa kwa UNMISS kuingia Yei akisistiza kwamba

(SAUTI YA YASMINA)

“Kwa hakika hakuna suluhisho la kijeshi kwa hali ya Sudan Kusini, ni lazima tuketi kwenye majadiliano na watu ni lazima waruhusiwe kuendelea na kazi zao za kila siku na uhasama lazima ukome”