Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya biashara EAC iimarishe ushirikiano wa kikanda- Kituyi

Sekta ya biashara EAC iimarishe ushirikiano wa kikanda- Kituyi

Katibu Mtendaji wa kamati ya kimataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi ametaka sekta ya biashara kwenye ukanda huo ichagize upatikanaji wa fursa za ajira na kuimarisha ushirikiano wa kikanda.

Amesema hayo katika mkutano wa siku tatu wa Baraza la biashara la nchi za Afrika Mashariki, EABC uioanza leo jijini Nairobi Kenya ukienda sambamba na maonyesho ya wajasiriamali.

Dkt. Kituyi amesema teknolojia inachagiza maendeleo ya sekta hiyo akitolea mfano wa Mpesa Kenya na RSwitch ya Rwanda.

Hata hviyo amesema fursa hizo ziweke mazingira ya fursa za ajira na kuimarisha ushirikiano wa kikanda.

Halikadhalika ametaka baraza hilo la biashara Afrika Mashariki liangazie ni kwa jinsi gani nchi wanachama zinaweza kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya teknolojia wakati huu ambapo matumizi ya roboti yanaweza kuengua ukanda huo katika kujinasibu kuhimili ushindani kwa minajili ya kuwepo kwa gharama ndogo za uajiri.

Afrika Mashariki inaundwa na Kenya, Tanzania, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini.