Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni miaka 20 tangu kuanzishwa mahakama ya kimataifa ya sheria za masuala ya bahari

Leo ni miaka 20 tangu kuanzishwa mahakama ya kimataifa ya sheria za masuala ya bahari

Katibu mkuu Ban Ki-moon amesema tangu kuanzishwa kwa mahakam ya kimataifa ya sheria ya masuala ya bahari miaka 20 iliyopita , mahakam hiyo imeweza kushughulikia kesi 25. Akizungumza katika hafla maalumu ya maadhimisho ya miaka 20 ya mahakama hiyo mjini Hamburg nchini Ujerumani, Ban amesema mahakam hiyo ni kipengele muhimukatika kuheshimu na kufuta asheria za masuala ya bahari.

Amesema kwa miaka mingi wafanyabiashara wamekuwa wakitumia mji wa Hamburg kwenye mdomo wa Mto Elbe kama mahali kiungo na upande wa kaskazini mwa Ulaya na maeneo mengine ya dunia kwa njia ya biashara ya bahari ambayo imeufanya mji huo kuwa bunifu na maarufu.

Ameongeza kuwa mahakam hiyo ina jukumu muhimu katika utekelezaji wa ajenda kwa maendeleo ya 2030 hususani katika kuahakikisha utekelezaji wa lengo nambari 14 linalotilia mkazo masuala rasilimali na viumbe vya baharini, ikisisitiza utekelezaji wa sheria za kimataifa , kama ilivyoainishwa kwenye sheria za masuala ya bahari za Umoja wa Mataifa.

Na kuhakikisha kuwa matumizi ya binadamu ynakwenda sanjari na rasilimali za baharini , Ban amesema kuna mengi ya kufanya kuleta uwiano huo na hasa kuzingatia vipengee vilivyoorodheshwa kwenye mkataba.

Amepongeza mahakama hiyokwa maadhimisho na juhudi zake za kuendelea kuhamasisha matumizi ya amani na uendelevu baharini kote duniani.

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Rais wa Mahakama hiyo Vladimir Vladimirovich Golitsyn, Rais wa Ujerumani Joachim Gauck na Meya wa Jiji la Hamburg Olaf Scholz.