Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio dhidi ya askari wa Niger

Ban alaani shambulio dhidi ya askari wa Niger

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio dhidi ya askari wa Niger waliokuwa lindoni katika kituo cha wakimbizi wa ndani huko Tazalit, jimbo la Tahoua nchini Niger.

Katika shambulio hilo askari 22 wa jeshi la Niger waliuawa na wengine ambao idadi yao haikutajwa walijeruhiwa.

Ban kupitia msemaji wake ametuma salamu za rambirambi kwa wafiwa na serikali ya Niger na wananchi huku akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Ametoa wito kwa mamlaka za Niger kusaka na kuwafikisha mbele ya sheria watuhumiwa wa tukio hilo.

Amesishi serikali ya Niger kuimarisha usalama na ulinzi kwenye maeneo ya wakimbizi na makundi mengine yaliyo hatarini zaidi