Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kimbunga Matthew kimeathiri vibaya jamii Haiti:OCHA

Kimbunga Matthew kimeathiri vibaya jamii Haiti:OCHA

Baadhi ya jamii Kusini mwa Haiti zimesambaratishwa kabisa na kimbunga Matthew kilichokumba taifa hilo la Caribbean Jumanne, kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA.

Duru zimetaja idadi ya waliopoteza maisha kwenye zahma hiyo kufikia 500, huku milioni 1.2 kuathrika na wengine 350,000 wakihitaji msaada wa kibinadamu.

Enzo di Taranato ni mkuu wa OCHA ofisi ya Haiti anaelezea hali halisi kwa jamii zilizoathirika.

(SAUTI YA ENZO)

Baadhi ya jamii karibu zimesambaratishwa kabisa na upenpo mkali, hivyo malazi, huduma ya usafiri wa umma, shule, hospitali vimeathirika. Kuna uharibifu mkubwa kwenye mfumo wa umeme na mfumo wa maji, hivyo na hali ni ngumu sana inayozikabili jamii zilizoathirika na kimbunga Matthew.”