Skip to main content

UNHCR imeshtushwa na shambulio lililoua askari 22 wa Niger wanaolinda wakimbizi wa Mali:

UNHCR imeshtushwa na shambulio lililoua askari 22 wa Niger wanaolinda wakimbizi wa Mali:

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limeshtushwa na kusikitishwa na shambulio lililofanywa na watu wasiojulikana kwenye makazi ya wakimbizi wa Mali mjini Tazalit jimbo la Tahoua Niger mpakani na Mali.

Tukio hilo lililotokea jana Oktoba 6 limekatili maisha ya askari 22 wa jeshi la Niger na kujeruhi wengine watano. Askari hao walikuwa wakishika doria kwenye makazi hayo yanayohifadhi wakimbizi 4,000 kutoka Mali.

Hakuna mkimbizi aliyepoteza maisha au kujeruhiwa , na UNHCR imelaani vikali tukio hilo dhidi ya watu wanaohakikisha usalama kwa wakimbizi kama anavyofafanua msemaji wa UNHCR William Spindler

(SAUTI YA SPINDLER)

"UNHCR inalaani vikali shambulio dhidi ya wafanyakazi wanaohakikisha usalama kwa wakimbizi wa Mali walio katika mazingira magumu zaidi, wakimbizi ambao wamelazimika kukimbia makwao baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokea mwaka 2012"