Uchunguzi unahitajika kufuatia ghasia Ethiopia:UM

7 Oktoba 2016

Uchunguzi unahitajika kufuatia ghasia zilizozuka kwenye jimbo la Oromia kusini Mashariki mwa Addis Ababa Ethiopia tangu Jumapili iliyopita.

Wito huo umetolewa na ofisi ha haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikitaja kuwa watu wengi wamepoteza maisha baada ya kuanguka kwenye mitaro na ziwa Arsede wakikimbia askari wa usalama waliokuwa wakiwafurusha waandamanaji kwenye tamasha la kidini mjini Bishoftu.

Kwa mujibu wa ofisi hiyo maandamano yamechochewa na watu kutokuwa na imani na serikali, takwimu za idadi ya vifo na vitendo vya askari wa usalama. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

“Kuna haja ya kufanyika kwa uchunguzi huru aili kujua nini hasa kilitokea Jumapili iliyopita, na kuhakikisha uwajibikaji kwa vitendo hivi na matukio mengine ya tangu Novemba mwaka jana yaliyohusisha maandamano yaliyomalizika kwa ghasia”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter