Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fahamu mchakato wa kumpata Katibu Mkuu wa UM

Fahamu mchakato wa kumpata Katibu Mkuu wa UM

Vigezo

Kwa mujibu wa ibara ya 97 ya Katiba ya Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu atateuliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kufuatia pendekezo la Baraza la Usalama. Kwa maneno mengine ibara hiyo ya 97 inaweka ngazi mbili za mchakato: Mosi ni pendekezo la Baraza la Usalama na pili ni uamuzi wa Baraza Kuu.

Mtu anaweza kuhoji je inawezekana Baraza la Usalama kupendekeza kwa Baraza Kuu zaidi ya mgombea mmoja?

Ni kwamba ingawa Katiba haizuii Baraza la Usalama kupendekeza jina zaidi ya moja, azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa namba 11 (i) la tarehe 24 Januari mwaka 1946 linaeleza kuwa ni vema Baraza la Usalama likawa mthibitishaji wa mgombea mmoja pekee na hiyo imekuwa utamaduni tangu wakati huo hadi sasa anaposakwa Katibu Mkuu wa Tisa.

Utaratibu wa Baraza la Usalama kutoa pendekezo la jina.

image
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.(Picha:UM/JC McIlwaine)
Baraza la Usalama hupitisha azimio linaloweka pendekezo. Azimio hilo limekuwa likipitishwa katika kikao cha faragha kwa kuwa kanuni ya 48 ya taratibu za Baraza la Usalama inaeleza kuwa pendekezo lolote kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu uteuzi wa Katibu Mkuu unapaswa kujadiliwa katika kikao cha faragha.

Katika wakati ambao kuna wagombea kadhaa ambao wanapaswa kujadiliwa, Baraza hupiga kura kabla ya kupitisha azimio lake. Na katika miaka ambayo mgombea ni mmoja tu, basi utaratibu wa Baraza ni kuendelea bila kupiga kura na kupitisha azimio ambalo mara nyingi hupita kwa kauli moja.

image
Baraza Kuu.(Picha:UM/Eskinder Debebe )
Mchakato wa sasa ulikuwa na wagombea 13 wanawake Sita, wanaume Saba ambapo katika safari ya mchakato, watatu walijitoa ambao ni Christiana Figueres, Prof. Dr. sc. Vesna Pusiæ na Dr. Igor Lukšiæ