Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya 300,000 wahitaji msaada Haiti baada ya kimbunga Matthew

Watu zaidi ya 300,000 wahitaji msaada Haiti baada ya kimbunga Matthew

Watu takriban 350,000 wanahitaji msaada wa kibinadamu Haiti baada ya kimbunga Matthew kukumba kisiwa hicho wiki hii.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, misaada bado haijaweza kuwafikia waathirika wengi kutokana na matatizo ya miundombinu ikiwemo moja ya daraja kubwa ambalo limevujika kutokana na kimbunga hicho.

Enzo di Taranto, mkuu wa ofisi ya OCHA Port-au-Prince amesema kimbunga kimeathiri eneo zima la la Kusini mwa nchi hiyo na jana kimepiga katika eneo la Kaskazini Magharibi. Kumekuwa na uharibifu mkubwa ikiwemo kupotea maisha ya watu , lakini hofu nyingine ni pamoja na kipindupindu, makambi ya muda ambayo ni makazi ya maelfu ya watu walioathirika na tetemeko la 2010 na Wahaiti wanaorejea kutoka Jamhuri ya Dominikan. Ameongeza kuwa...

(SAUTI YA ENZO)

“Hadi usiku wa Oktoba 5, tunakadiria kwamba watu milioni 1.5 wameathirika huku wengine 350,000 wakihitaji msaada wa kibinadamu. Leo timu ya tathimini ya masuala ya majanga na endapo hali ya hewa na usalama vikiruhusu itakwenda nje kutathimini hali. Wazo ni kuanzisha vituo viwili vya operesheni kwa ushirikiano na MINUSTAH kimoja Les Cayes na kingine Jeremie”