Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuanza kwa utekelezaji wa mkataba wa Paris kwapongezwa

Kuanza kwa utekelezaji wa mkataba wa Paris kwapongezwa

Rais wa Baraza Kuu Peter Thomson amepongeza hatua ya kuanza kwa utekelezwaji wa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi mnamo Novemba nne mwaka huu. Rosemary Musumba na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ROSEMARY)

Hatua hii inafutia vigezo vilivyokuwa vinahitajika kuvukwa,  ambavyo ni kinachotaka nchi zilizoridhia mkataba ziwe zinachangia asilimia 55 ya hewa chafuzi inayotolewa duniani, na nchi 55 zinazochafua zaidi hewa duniani kuridhia ambapo sasa jumla yao ni 73.

Amempongeza Katibu Mkuu kwa jitihada zake za kuhakikisha hatua za mabadiliko ya tabianchi zinchukuliwa na wadau wote kutokana na umuhimu wake katika agenda ya maendeleo ya 2030.

Kwa upande wake Katibu mkuu mtendaji wa mkataba wa Umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi (UNFCCC), Patricia Espinosa amenukuliwa akisema huu ni wakati wa historia kwa watu wote duniani na kwamba kasi iliyotumiwa na nchi katika kuuingiza mkataba huo katika utekelezaji ni ya kipekee katika uzoefu wa makubaliano ya kimataifa.

Bi Espinosa  amesema kasi hiyo ni udhihirisho wa umuhimu wa makabiliano ya mabadiliko ya tabianchi ambayo mataifa yaliyojikita kwayo kwa kutambua fursa za mkataba wa Paris.