Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua lazima zichukuliwe sasa kuinurusu Aleppo:De Mistura

Hatua lazima zichukuliwe sasa kuinurusu Aleppo:De Mistura

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu Syria Staffan de Mistura amesema Syria iko katika hali ya hatari na hususani Aleppo baada ya wenyeviti wawili kuamua kusitisha majadiliano.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva amesema hatua hiyo ya Marekani na Urusi inazidi kuuweka njia panda mustakhbali wa amani ya Syria na si haki kwa raia wa nchi hiyo ambao wameshateseka vya kutosha.

Hata hivyo amesisitiza kwamba kikosi kazi cha kimataifa kwa ajili ya Syria ISSG, kitaendelea kukutana kusaka suluhu.

(SAUTI DEMISTURA)

“Tuko katika hali ya hatari, tuwe wazi, kuhusu Syria, kuhusu Aleppo na kuhusu mustakhbali wa nchi hii. Ukweli kwamba Urusi na Marekani wanafanya maamuzi yao kusitisha mazungumzo ya sasa , hakutaathiri uwepo wa ISSG”