Skip to main content

Hali ya watoto wakimbizi wa Burundi kambini Tanzania inaridhisha

Hali ya watoto wakimbizi wa Burundi kambini Tanzania inaridhisha

Mwakilishi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania Maniza Zaman na mwakilishi mkazi wa Burundi Bo Victor wamefanya ziara ya pamoja kwenye kambi za wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania.

Wawakilishi hao wamezuru kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtembeli zilizoko mkoani Kigoma nchini Tanzania . Zaidi ya nusu ya watoto wote kwenye kambi hizo ni wakimbizi kutoka Burundi. Maniza Zaman anafafanua lengo la ziara yao

(SAUTI YA MANIZA)

Likuwa ni kungalia hali katika kambi hizi za wakimbizilakini pia kuangalia upande wa serikali hapa kipaumbele chao na jinsi gani ya kuweza kuzisaidia jamii zinazowahifadhi. Na kilichonigusa Zaidi ni Kwamba asilimia karibu 60 ya wakimbizi hawa ni watoto, kwahiyo kwa UNICEF huu ni mgogoro kwa watoto”

Kwa upande wake mwakilishi wa Burundi Bwana Bo amesema hali walishoshuhudia katika siku tatu za ziara yao inaridhisha licha ya changamoto zilizopo na kubwa kwake ni suala la elimu kwa sababu

(SAUTI YA BO)

“Hapa kambini Tanzania mtaala wa elimu wa Burundi unaendelea kufutwa, kwa upande wa Burundi tunaweza kushirikiana na timu ya Tanzania, ili kuhakikisha vifaa vinavyohitajika kwa mtaala huo vinapatikana na watoto wana fursa ya kusoma na kuendelea katika elimu pia”