Ban aenziwa na Rais wa Afghanistan kwa tuzo ya heshima ya kijamii

Ban aenziwa na Rais wa Afghanistan kwa tuzo ya heshima ya kijamii

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametunukiwa tuzo ya ngazi ya juu kabisa ya kiraia nchini Afghanistan.

Rais wa nchi hiyo Ashraf Ghani amemkabidhi Bwana Ban tuzo hiyo ya Ghazi Amir Amanullah Khan, mjini Brussels.

Tuzo hiyo ambayo ni medali tukufu hutolewa na serikali ya Afghanistan kwa raia wa Afghanistan na watu wasio raia wa nchi hiyo kwa kuthamini huduma zao. Hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo imefanyika kandoni mwa mkutano kuhusu Afghanistan unaoendelea mjini Brussels.

Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 70, na mashirika 20 ya kimataifa wanashiriki katika mkutano huo wa ngazi ya juu ambapo Afghanistan inatanabaisha mtazamo wa mustakhbali wa taifa hilo na jumuiya ya kimataifa kuaihidi msaada wake wa kisiasa na kifedha kuhakikisha Amani, ujenzi mpyaq na maendeleo ya Afghanistan.