Shambulizi la meli kwenye pwani ya Yemen yalaaniwa: UM

5 Oktoba 2016

Shambulizi la meli inayomilikiwa na Muungano wa Emarati (UAE) kwenye pwani ya Yemen limelaaniwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Shambulio hilo la roketi lililofanywa na wapiganaji waasi wa kundi la Houthi Oktoba mosi, limeanguka kwenye meli hiyo mjini Bab al-Mandeb kwenye Ghuba ya Aden.

Muungano wa Emarati ni mshirika kwenye muungano wa nchi zinazoisaidia serikali ya Yemen katika mapambano yake dhidi ya Wahouthi, ambao wanadhibiti mji mkuu wa nchi hiyo Sana'a.

Katika taarifa yake baraza la usalama limesema wajumbe wake wanachukulia vitisho vyovyote vya usafiri wa meli katikia eneo hilo kwa umakini mkubwa.

Limesisitiza kwamba uhuru wa kusafiri kwa meli katika eneo la Bab al-Mandeb kwa mujibu wa sharia za kimataifa ni lazima uheshimiwe.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter